Wednesday, June 15, 2011

Bambo anusurika kifo, alazwa MOI

KUNA taarifa kwamba, msanii maarufu wa vichekesho kwenye luninga nchini Tanzania, Dikson Makwaya maarufu kwa jina la Bambo, amepata ajali jana usiku wakati anarudi nyumbani kwake Kigogo Darajani.


Kwa mujibu wa blog ya chini ya carpet, msanii huyo wa kundi la Ze Komedi linalorusha vichekesho vyake kituo cha EATV cha Dar es Salaam, alikumbwa na mkasa huo katika mzunguko wa Kigogo a.k.a Kigogo Round About akiwa kwenye pikipiki aka bodaboda wakati anakwenda home.


Bambo na dereva wake waligongwa na daladala aina ya Coaster na kwa mujibu wa blog hiyo, msanii huyo amevunjika mfupa wa paja, na amepata majeraha kichwani na mkononi.


Dereva hali yake taabani kidogo na kwa sasa Bambo yuko katika Kitengo cha Mifupa MOI, katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili anasubiri kufanyiwa upasuaji.


Ajali za pikipiki limekuwa ni tatizo sugu sanjari na madereva wa bodaboda kutekwa na kuuawa.

No comments:

Post a Comment