Thursday, May 26, 2011

Mume ajiua kwa risasi, amjeruhi mkewe

INADAIWA kuwa, miaka kadhaa iliyopita, mume wa Vicky aliuawa kwa kupigwa risasi, na sasa mumewe mwingine KAJIUA kwa kujipiga risasi mjini Dodoma.


Mke wa marehemu, Vicky Kaombwe (34) naye kapigwa risasi, kalazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma iliyopo mjini humo.


Polisi wamesema, mume wa Vicky, Ofisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino yenye makao yake jirani na Ikulu ndogo ya Serikali, nje ya mjini wa Dodoma, Fredy Kaombwe (28), amejiua kwa kijipiga risasi kichwani.


Kuna taarifa zinazodai kuwa, Fredy hakujipiga risasi kichwani ila kifuani.


Kwa mujibu wa Polisi, Fredy alijiua muda mfupi baada ya kumkuta mkewe akiwa na mwanamume mwingine baa mjini Dodoma.

Inadaiwa kuwa, baada ya kumkuta mkewe hapo baa, Fred alimkimbiza mkewe na walifika hadi nyumbani kwao, mtaa wa Madole , Kigamboni,mjini Dodoma, wakati Vicky akiwa katika harakati za kufungua geti akapigwa risasi iliyomjeruhi sehemu za mbavu.

Kuna taarifa kwamba, hali ya Vicky si nzuri, bado yupo hospitali.


Tukio hilo limekuwa gumzo mjini Dodoma kutokana na mazingira ya kifo cha mume wa Vicky wa awali na huyu wa sasa.

2 comments:

  1. si wa kuoa huyooo lol

    ReplyDelete
  2. unsolved mystery.Inaonekana yeye waume zake wanauawa tu.Na wanawake nao kama alikuwa bado anapenda kwingene ya nini kuolewa, something must be going on here. RIP FREDDY KAOMBWE.

    ReplyDelete