Tuesday, May 25, 2010

Liyumba afungwa miaka miwili jela

HATIMAYE miongoni mwa kesi zilizowahi kuwa na mvuto nchini 'kesi ya Liyumba' imekwisha.
Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam, imemuhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Benki Kuu Tanzania (BOT)kifungo cha miaka miwili jela.

Jopo la mahakimu waliosikiliza kesi hiyo jana lilitofautiana,Hakimu Edson Mkasimongwa alitofautiana na mahakimu wenzake, Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa.

Mlacha na Mwingwa walimwona Liyumba ana hatia lakini Mkasimongwa, alisema,Liyumba hana hatia.

Mkasimongwa alisema,mahakama ilishindwa kuthibitishiwa kama kweli alitumia madaraka yake vibaya katika ujenzi wa jengo pacha la BoT,Dar es Salaam.

Hata hivyo Mkasimongwa alisema kwa kuwa wengi wape, hukumu ambayo itahesabika kuwa ndio uamuzi wa mahakama.

1 comment:

  1. KWELI MUNGU ASHUKURIWE KWA JINSI TULIVYO, TUNAZAA WATOTO WAKIWA WAZIMA NA WAMEKAMILIKA, NIMEONA HURUMA HATA SIELEWI NIMWAMBIEJE MUNGU KWA HILI, MUNGU TUONDELEE HAYA!SIJUI ANACHEZAJE SASA NA WATOTO WENZAKE WANAMUONAJE NA YEYE ANAJISIKIAJE? OOH! GOD

    ReplyDelete