KUNA mdau kanitumia hayo utakayoyasoma hapo chini, wewe kwako vipi?
Kwangu na mama watoto (my wife wangu), simu zina mwenyewe kwa maana ya kutumia kwa wakati huo na pia kwa kuangalia nani aliichagua wakati inanunuliwa.
Vinginevyo nina uhuru wa kuigusa na kutumia simu yake 24/7 naye pia anashika na kutumia simu yangu wakati wowote.
Watu wote kwenye address book zetu wameingizwa kwa majina yao. Mimi nime-save jina la mke wangu kwa kutanguliza "my sweety wife....".
Pia mimi kanipa jina la "my darling husband". Mke wangu anatabia ya kufuta call records au sms lakini mara nyingi namwambia kuwa si vizuri kufuta zote kwa sababu inaweza kuleta mashaka yasiyo na sababu.
Kwa ujumla sijawahi kupata shida kuhusu simu yake naye hajawahi kuwa na tatizo na simu yangu.
Kwa hiyo naamini wanaoficha/wanaoweka vikwazo (embargo) kuhusu simu zao hawajiamini kwenye suala la uaminifu katika ndoa/mahusiano.
Vinginevyo sisi ndiyo hatufahamu maana ya hicho kitu kinachoitwa privacy kwenye simu ya mkononi.
Big up mkuu. Nimeikubali kzazi yako hakika unasitahili pongezi.
ReplyDeletewww.ajirazetu.blogspot.com
www.ilovetanzania.blogspot.com
www.harusiyetu.blogsopt.com
Keep up the good work!