Wednesday, December 2, 2009

Mfungwa atunukiwa shahada ya sheria

MKUU wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT),Dk John Malecela, amemtunuku mfungwa,Semayoga Ernest,Shahada ya Sheria.

Mfungwa huyo anayetarajia kumaliza kifungo Agosti mwakani ameiomba Serikali iwasamehe wafungwa waliojirekebisha.

Ameyasema hayo katika mahafali ya pili ya 21 yaliyofanyika jana katika Ukumbi wa KM, Ukonga jijini Dar es Salaam.

Ernest anatumikia kifungo cha miaka 10 katika gereza la Ukonga,Dar es Salaam,ana ndoto za kujiunga kwa shahada ya uzamili ya sheria.

Alifungwa baada ya kukamatwa akifanya biashara haramu ya dawa za kulevya nchini Malaysia mwaka 1999.

Ernest amesema,aliamua kusoma sheria ili kusaidia wafungwa kwa kuwa hawafahamu haki na taratibu za kuwasaidia kuandaa rufaa zao.

No comments:

Post a Comment