Friday, September 25, 2009

Bomu laua watoto wawili Mbagala

BOMU lililolipuka Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam jana asubuhi, limeua watoto wawili wenye umri wa miaka sita.
Mlipuko huo ulijeruhi watoto watatu, mmojawao, Stella Chawala, hali yake ni mbaya, amelazwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dar es Salaam.
Watoto waliopoteza maisha ni Regina Chawala na Rajab Saidi,wengine waliojeruhiwa ni Asha Selemani, na Sada Selemani.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, wamethibitisha kutokea kwa mlipuko huo.
Taaarifa ziliopatikana katika eneo la tukio zimedai kuwa, bomu hilo lililipuka saa 1.30 asubuhi wakati watoto hao wakicheza jirani na sehemu ulipotokea mlipuko.

No comments:

Post a Comment