Monday, August 3, 2009

JK azindua rasmi Kilimo Kwanza

Sekunde chache zilizopita Rais Dk Jakaya Kikwete amezindua rasmi azimio la KILIMO KWANZA.
Rais pia amefungua rasmi maonyesho ya Nane Nane kitaifa.
Rais ameyafanya hayo katika viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Azimio la Kilimo Kwanza litatekelezwa sanjari na mpango wa taifa wa kuboresha sekta ya kilimo(ASDP).
Dk Kikwete amesema, Kilimo kwanza si mbadala wa ASDP au Mpango wa Taifa wa kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA)
Rais na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bado wapo kwenye viwanja hivyo.

No comments:

Post a Comment