Taarifa za kifo cha Koplo Josephat Milambo zinasikitisha, si tu kwa kuwa amepoteza maisha kwa sababu ya majeraha aliyopata katika tukio la ujambazi, ameacha mjane na watoto watano, mmoja wao ana miezi saba.
Msemaji wa familia ya marehemu, Salvatory Kateka, amekaririwa akisema, kwa namna alivyokuwa ameumia, walikataa tamaa tangu siku ya tukio wiki iliyopita.
Koplo Josephat aliumia wakati majambazi yalipovamia benki ya NMB Temeke, wakapora sh milioni 61, na kuua askari wa kampuni ya ulinzi.
Katika tukuo hilo, polisi huyo alikatika mguu, vidole vitatu vya mkono wa kulia, na aliumia pia sehemu ya makalio.
Aliaga dunia juzi katika wodi ya wagonjwa mahututi kwenye Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI)
No comments:
Post a Comment