Saturday, February 21, 2009

Liyumba yupo wapi?


Amatus Liyumba

YEYE na mwenzake, Deogratius Kweka wanashitakiwa kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 200.

Liyumba alipewa dhamana iliyozua utata kwa kuwa hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Khadija Msongo, aliruhusu mshitakiwa huyo awe nje kwa dhamana ya sh milioni 882 tu wakati mwanzo alitakiwa kudhaminiwa kwa fedha taslimu sh bilioni 55 au mali zisizohamishika zenye thamani hiyo.

Siku moja baadaye mshitakiwa huyo alitakiwa mahakamani tena lakini hakuonekana, na hadi sasa anatafutwa.

No comments:

Post a Comment