Monday, February 23, 2009

Liyumba bado kitendawili


Amatus Liyumba(kulia)

KUNA taarifa zinazodai kuwa mmoja wa watuhumiwa wawili katika mashitaka ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 200, Amatus Liyumba amepatikana.

Hadi sasa hakuna mamlaka yoyote ya Serikali iliyothibitisha taarifa hizi, kitendawili kitateguliwa kesho kwa kuwa ndiyo siku aliyopangiwa kufika tena mahakamani.

Liyumba aliachiwa kwa dhamana iliyozua utata na hadi sasa mengi yanasemwa mitaani kuhusu dhamana hiyo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment