Tuesday, February 24, 2009

Liyumba atinga Kisutu

MMOJA wa washitakiwa katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 200, Amatus Liyumba leo amevunja ukimya na kubatilisha taarifa kuwa alitoroka baada ya kupewa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Liyumba alifika mahakamani hapo leo asubuhi, kesi ikaendelea kama kawaida huku kukiwa na mabishano kati ya mawakili wa Serikali na wale wa washitakiwa.

Hadi saa saba mchana leo mahakama ilikuwa haijatoa uamuzi kuhusu dhamana lakini hisia za wengi ni kwamba huenda Liyumba atarudi rumande kwa kuwa mawakili wa Serikali wamedai kuwa kitendo chake cha kuwasilisha mahakamani hati ya kusafiria iliyokwisha muda wake huku akiwa na hati nyingine kimeonyesha kuwa si muaminifu.

No comments:

Post a Comment