MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imefuta dhamana iliyotoa kwa mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya sh bilioni moja.
Amatus Liyumba jana alifika katika mahakama hiyo hivyo kumaliza uzushi kuwa alitoroka baada ya kujidhamini siku kadhaa zilizopita.
Mahakama imebaini kuwapo kwa makosa 10 katika hati alizowasilisha kwa ajili ya maombi ya dhamana ikiwa ni pamoja n akuwapo kwa majengo yanayofanana na inazitilia shaka hati hizo.
Mshitakiwa huyo pia aliwasilisha mahakamani hati ya kusafiria iliyokwisha muda wake, lakini imebainika kuwa ana hati nyingine ya kusafiria aliyoipata mwaka 2005, itakwisha muda wake 2015.
Liyumba alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Benki kuu Tanzania(BoT), yeye na mwenzake, Deogratius Kweka wanatuhumiwa kuidhinisha mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya taasisi hiyo ya Serikali bila idhini ya bodi ya BoT hivyo kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni 200.

Majengo hayo yapo Dar es Salaam, Liyumba atapandishwa kizimbani Machi 10 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment