Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
WABUNGE wa Bunge la Tanzania wameikataa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amemuomba Spika wa Bunge, Anne Makinda Serikali ipewe wiki tatu ikaiandae upya bajeti hiyo, Makinda amekubali.
Makinda ameafiki uamuzi wa wabunge kuikataa bajeti hiyo kwa maelezo kuwa Wizara hiyo ni nyeti, na kwamba, kukosekana kwa umeme kunawaathiri sana Watanzania.
Wakati waanachangia bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wabunge wengi walisema hawaiungi mkono hasa kutokana na tatizo la umeme.
Wabunge wanasema, hawataki kusikia orodha ya miradi ya umeme, wanataka UMEME.
No comments:
Post a Comment