Wednesday, August 5, 2009

Waziri Mkuu wa Russia akijivinjari

Si kawaida kuona viongozi wakuu wa nchi za Afrika wakiendesha farasi au wakiwa vifua wazi, au wakiogelea.
Kwa Putin ni jambo la kawaida, kuna wakati alipigwa picha anavua samaki akiwa kifua wazi.
Rais huyo Mstaafu wa Russia kapigwa picha hizi akiwa mapumzikoni nchini Siberia.

Umewahi kumuona Waziri Mkuu anaogelea?

Putin anakumbuka enzi zake akiwa active kwenye masuala ya jeshi, anamudu mambo hayo, siasa, na hivi karibuni ametoa CD yake akicheza Judo.

Ni nadra kupata picha kama hii ikimuonyesha Waziri Mkuu ambaye pia ni Rais Mstaafu. Putin alikuwa Rais wa Russia mwaka 2000 hadi 2008
Baada ya kupanda miti, kupanda farasi, kuogelea na mazoezi mengine sasa ni 'mlo time'.
Waziri Mkuu Putin anapata mlo nyumbani kwa mwanakijiji.
Naona ni jambo zuri tukiona na picha za viongozi wetu wakiwa kwenye hali kama hii, natural & simple.
Si vibaya siku moja tukiona picha ya JK anawinda Serengeti kwa kuwa naamini wengi watapenda kuiga hivyo mapato ya utalii wa uwindaji yataongezeka.
Bodi ya Taifa ya Utalii(TTB) mpo wapi? kwa nini msiwashauri viongozi wetu mambo kama haya?
Kuna ubaya gani nikimuona JK anaonekena vipi akiwa mapumzikoni mbugani?
Nafahamu kwamba mara nyingi huwa anakwenda huko, kwa nini TTB msiwashauri IKulu wakaruhusu picha zinazopigwa huko zitumike kuhamasisha utalii wa ndani?
Kwa mtazamo wangu itapendeza pia tukiona picha ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa juu ya mti katika hifadhi ya Katavi, Rukwa akiangalia mandhari ya eneo hilo.
Itakuwa bomba pia wananchi wakiona Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein akiwa amevaa mavazi simple akiwa mapumzikoni kwenye moja ya maeneo ya hifadhi za taifa.
Zitakuwa picha nzuri kwa kuwa tumezoea kuwaona wamevaa suti na tai.

No comments:

Post a Comment