Tuesday, August 11, 2009

Ronaldo asababisha zogo Night Club

Askari wakimzuia mpenzi wa zamani wa Christiano Ronaldo, Nereida Gallardo asimfikie mwanasoka huyo.

Ronaldo alimchunia kabisa Nereida, juhudi za msichana huyo kumuita hazikuzaa matunda, alijifanya hamuoni.

Ili akuondokana na bughudha hizo, Ronaldo na rafiki yake ( Mwenye fulana ya mistari) waliamua kuondoka katika club hiyo iliyopo kwenye kisiwa cha Majorca nchini Hispania.

Msichana huyo alipania kuzungumza na Ronaldo, alimfuata hadi nje, mwanasoka huyo 'alimfungia vioo', askari nao walimzibia, basi tena!

Mwezi kama huu mwaka jana, Ronaldo na Nereida walikuwa 'wanakula good time' nchini Italia.
Nereida amekuwa akikanusha kuwa ameachana na Ronaldo.
Inawezekana msichana huyo bado anampenda mwanasoka huyo lakini duh, jamaa ndo kama hivyo.
Sakata hilo lilitokea usiku wa Jumapili ya wiki iliyopita

No comments:

Post a Comment