Saturday, August 8, 2009

Mtikila kizimbani

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (45) jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa mkoa wa Mwanza kujibu mashitaka sita.

Mtikila anadaiwa kutoa taarifa za kugushi zilizolenga kupatiwa kibali cha kuitisha mkutano katika eneo la Magomeni Kirumba.

Mtikila na mchungaji mwenzake, Eliud Rwehumbiza(41) wa jijini Mwanza wanadaiwa kutoa maelezo ya uongo kwa nyakati tofauti kwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow.

No comments:

Post a Comment