Saturday, March 14, 2009

Aliyempiga Mwinyi jela mwaka mmoja


KIJANA aliyempiga kofi Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi leo ameanza siku ya pili jela, kafungwa mwaka mmoja.

Hakimu Mkakzi wa Mahakama ya Kisutu, Neema Chusi alimhukumu kifungo hicho jana kwa kuwa kijana huyo, Ibrahim Said alikiri kosa na kukubali adhabu.

'Mimi ni kiumbe dhaifu, labda nissiombe Mahakama ila nimwombe Mwenyezi MunguSubhhna Wataallah kama tataka nitapunguziwa adhabu" alisema kijana huyo mahakamani.

No comments:

Post a Comment