Wednesday, February 18, 2009

Mshindi BSS bado yupo yupo


KINARA wa shindano la kusaka vipaji vya wanamuziki, maarufu kama Bongo Star Search(BSS) la mwaka jana, Misoji Nkwabi amekuwa kimya kwa muda mrefu lakini huenda utaanza kumsikia muda si mrefu.
Nimewasiliana naye leo akanieleza kuwa bado yupo kwenye game, amemaliza kurekodi albamu hivyo anajiandaa kuiingiza sokoni.
Misoji amesema alikuwa kimya kwa kuwa alikuwa akijiandaa kufanya mtihani wa kidato cha sita, na ameshamaliza kufanya mtihani huo hivyo sasa yupo free.

No comments:

Post a Comment